AMF Yatoa Taulo 3,000 za STARA kwa Wafungwa Wanawake Tanzania Bara na Visiwani Katika Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Asma Mwinyi Foundation (AMF) imeendelea kutekeleza jukumu lake la kuunga mkono heshima, afya na ustawi wa wanawake nchini kupitia kampeni ya kimataifa ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia. Katika kuadhimisha siku hizi muhimu, AMF imetoa jumla ya taulo 3,000 za kike za kibaolojia – STARA, bidhaa ya kipekee na endelevu iliyotengenezwa chini ya AMF, kwa ajili ya wafungwa wanawake katika Magereza ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Hatua hii inalenga kuboresha mazingira ya afya ya wanawake gerezani na kuhakikisha wanapata mahitaji ya msingi ya utu na usafi wakati wanapokabiliana na changamoto za kifungo.
Mwanzilishi wa AMF, Mhe. Asma Ali Hassan Mwinyi (FCCA), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Welezo, ameendeleza utamaduni wake wa kuwatembelea na kuwapatia mahitaji muhimu wanawake walioko magerezani. Mbali na taulo za kike za STARA, AMF imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
